Radio Fadhila
Radio Fadhila
09/03/2026, 13:03

Na Lilian Martin
Wakati mwingine tunaamini kwamba watu wengi huishi maisha kutokana na yale walitopitia hali hiyo tunaiona kwa watu wanaofanya matendo ya huruma ya kuhudumia wenye mahitaji kutokana na ugumu aliouona kwa watu wa karibu
Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Leonard Akwilapo, amekabidhi baiskeli kumi kwa watu wenye ulemavu katika Jimbo la Masasi Mjini, wilayani Masasi.
Msaada huo unalenga kurahisisha usafiri na kuwasaidia walengwa hao kutekeleza shughuli zao za kila siku pamoja na kujiongezea kipato

Aliendelea kusema kuwa hii ni historia ndefu kuhudumia watu wenye uhitaji
Akwilapo amesema serikali na viongozi wana wajibu wa kuendelea kuwasaidia na kuwawezesha watu wenye ulemavu ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya jamii.