Radio Fadhila
Radio Fadhila
07/03/2026, 09:30

Lengo kubwa la Wanawake hawa wa Masasi wakiungana katika maombi na wanawake wengine ni kukumbushana majukumu ya Wanamke katika maisha ya kila siku na kumtegemea Mungu katika nyakati zote ili jamii iwe sawa
Na Lilian Martin
Wanawake wa wakikristo kutoka Madhehebu Mbalimbali Wilayani Masasi wameungana kwa pamoja kuadhimisha siku ya Maombi Duniani huku kauli mbiu yao ikiwa ni “Tupeleke Mizigo”
Maadhimisho hayo yaliyofanyika Katika kanisa la Rc Magumuchila yaliyohudhuriwa na wanawake kutoka madhebebu mbalimbali yamelenga kuwakumbusha wanawake juu ya majukumu yao na kudumu katika maombi ili kuijenga jamii yenye kumjua Mungu

na kwaupande wake Mwenyekiti msaidizi wa umoja wa Wanawake Bi Veronika Mkwatile alieleza namna alivyo barikiwa na makutano hayo ya pamoja na wamama wenzake

Sambamba na hayo Wanawake walikumbushana kuhusu kukemea maswala ya ukatili wa kijinsia na kuwaombea watoto katika jamii ili kuondokana na Wimbi la Ushoga
