Radio Fadhila
Radio Fadhila
29 September 2025, 12:28 AM

Katika kuendelea kuunga mkono jitihada za Taasisi za Elimu nchini wamama wa UMAKI Kanisa Anglikana mtaa wa lindi wamefanya ziara ya kutembelea shule ya rondo seminary na kuwapelekea zawadi wanafunzi shuleni hapo ikiwa imeambanata ,chakula pamoja na fedha kuajili ya kusapoti maendeleo ya shule.
Na kwaupande wake Mkuu wa Shule Bwn Linus Burian aliwashukuru wa mama wa Umaki kwa moyo wa kujitoa na kuona haja ya kuunga mkono maendeleo wa shule hiyo kwa kuwakumbuka watoto.

Sambamba na kushukuru Mkuu wa shule aliwataka wazazi kuendelea kuwa mabalozi wazuri kuitangaza shule ya Rondo na kuwapeleka vijana wao katika shule hiyo kwa ajili ya elimu, maadili,na maarifa.
