Radio Fadhila

Wanafunzi waanzilishi wakutana na kurudisha shukrani Rondo

14 September 2025, 6:14 PM

Wanafunzi waliowahi kusoma shule Rondo

Kuzaliwa mwanaume ni zawadi ila kuwa mwanaume ni maamuzi..msemo huu ukimaanisha kuwa mwanaume ni kutambua majukumu yanayo kupasa na kuyafanyia kazi.

Ni katika maafali ya 24 yaliyofanyika shule ya wavulana Rondo Junior Seminar iliyopo Mtama Mkoa wa Lindi ambapo na mgeni rasmi ni mkurugenzi wa halmashauri wilaya ya Mtama mhe: Andason Devid Msumba na kuwakutanisha vijana watano waliowahi kusoma katika shule hiyo wakati inaanza.

Mahudhurio ya Vijana hayo yalibeba shukurani kwa viongozi wa kanisa Anglikana kwa maono ya kuanzisha shule hiyo,kwa kutambua changamoto walizowahi kupitia wakati wakuanzishwa shule hiyo walichangia kiasi cha pesa kwa ajili ya shughuli za maendeleo zinazoendelea shuleni hapo

Wakizungumza wakati wa kuchangia

Si elimu tu tuliyoipata hapa shule ya Rondo bali maalifa,juhudi,kujituma,na namna ya kukabiliana na changamoto na sio kuzikimbia hii imetufanya kujivunia kaulimbiu ya sala na kazi. alisema mmoja wa vijana hao

Mmoja wao akiwa anazungumza

na kwa upande wake mkuu wa Shule ya Rondo Bwn Linus Burian alizungumza na waliohudhuria maafali hayo na kuwataka kutambua wajibu wao kama wazazi ni kumuandalia mtoto kesho iliyonjema.

Mkuu wa shule akiwa anazungumza

utakapo mleta mtoto shule ya Rondo anaandaliwa kuwa kijana kamili kiakili kimwili na kifikra,mazingira ya shule nirafiki kujifinzia kwakuwa jographia ya shule ni sehemu tulivu na hakuna usumbufu wa aina yoyote. Alisema mkuu wa shule

Ifahamu shule ya Rondo junior seminar