Radio Fadhila
Radio Fadhila
1 June 2025, 5:24 PM

Panya wanaoliwa si wale wanaoishi ndani ya nyumba bali wanaishi porini na wana lishe bora kutokana na kuharibu mazao ambayo mara nyingi wanakula viini ambavyo kitaalam ndivyo vina lishe.
Na Neema Nandonde
Kumekuwa na simulizi nyingi kuhusu vyakula vya asili ambavyo wakati mwingine unaweza kujiuliza ilikuwaje mpaka jamii husika wakaanza kula vyakula hivyo.
Kwa kabila la Wamakua linalopatikana wilayani Masasi mkoani Mtwara, miongoni mwa vyakula vyao vya asili ni upupu na kuna wakati mnyama panya anatumika kama kitoweo.
Chifu wa jamii ya Wakapa kutokea kijiji cha Lupaso wilayani Masasi, Chifu Mkonona Mkapa wa Tano ameeleza sababu za kuanza kuliwa chakula cha upupu na mnyama panya kufanywa kitoweo.
