Radio Fadhila
Radio Fadhila
12 May 2025, 2:12 PM

Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro uliotokana na tuhuma za wizi, ambapo mtuhumiwa alimshuku marehemu kuwa anamuibia baadhi ya vitu vyake.
Na Lilian Martin
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamshikilia mtu mmoja aitwaye Wales Gerald (45), mkazi wa Kijiji cha Mkarango, Wilaya ya Masasi kwa tuhuma za mauaji ya Daniel Raphael Roben (48).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Aprili 20, 2025 na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Mtaki Kurwijila amesema tukio hilo la mauaji lilitokea Machi 18, 2025 ambapo mtuhumiwa alimchoma marehemu kwa kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake, kisha kumkata sehemu zake za siri na kumsababishia majeraha makubwa yaliyopelekea kifo chake.
Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro uliotokana na tuhuma za wizi, ambapo mtuhumiwa alimshuku marehemu kuwa anamuibia baadhi ya vitu vyake, ambapo wawili hao walikuwa wakiishi nyumba moja na kushirikiana katika shughuli za kutafuta riziki.
Aidha jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo huku mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi kwa hatua zaidi za kisheria.