Radio Fadhila
Radio Fadhila
10 March 2025, 3:02 PM

Bandari ya Mtwara baada ya maboresho makubwa yaliyofanywa na serikali. Picha na Google
Meli hiyo ni moja kati meli nne, ambazo zinatarajiwa kuwasili bandarini hapo mwezi huu wa tatu hadi wa nne, zikileta salpha kwa ajili ya kukuza uzalishaji wa zao la korosho.
Na Neema Nandonde
Bandari ya Mtwara mkoani Mtwara, imepokea meli ya kwanza kati ya nne ambazo zinatarajiwa kuleta viuatilifu kwa ajili ya kukuza uzalishaji wa zao la korosho nchini, kwa msimu wa mwaka 2025/2026.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Bandari Ferdinand Nyath, amesema meli hiyo imewasili leo Jumatatu March 10, 2025 ikiwa imebeba viuatilifu maarufu kama salpha tani 9,202.
Amesema meli hiyo ni moja kati meli nne ambazo zinatarajiwa kuwasili bandarini hapo mwezi huu wa tatu hadi wa nne, zikileta salpha kwa ajili ya kukuza uzalishaji wa zao la korosho.
Kwa upande wake Mkurungezi wa Bodi ya Korosho (CBT), Francis Alfred amesema tani 40,000 za viuatilifu vya Korosho, zinatarajiwa kuletwa kwa ajili ya kukuza zao la korosho msimu wa 2025/2026.
Amesema serikali ilitoa maelekezo kwa wazabuni wa viuatilifu hivyo kusafirisha viuatilifu hivyo kupitia Bandari ya Mtwara.