Radio Fadhila
Radio Fadhila
8 March 2025, 9:58 PM

ni katika maandamano ya pamoja
Wanawake wilayani Masasi mkoani Mtwara wameadhimisha Siku ya Maombi ya wanawake katika kuombea taifa na mambo mbalimbali.
Katika maandamano hayo yaliyohusisha na mabango yenye jumbe inayosomeka (Nimeumbwa kwa namna ya ajabu) yenye lengo la kumfanya mwanamke kujithamini kwa namna alivyo.
Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya kanisa la Biblia Masasi, wanawake walipata wasaa wa kusikiliza neno la Mungu kutoka kwa mtoa neno aliyeandaliwa.
Moja ya mambo yaliyozungumzwa na mtoa neno ni kuwaasa wanawake kubeba mzigo kuombea taifa na jamii iliyowazunguka na kupinga ukatili wa kijinsia na kuacha tabia ya kujidharau wenyewe kutokana na jinsia zao na kujiona wa thamani kama wengine.