Radio Fadhila

Mfumo wa MMAMA unavyofanya kazi na mafanikio yake

14 December 2024, 12:13 AM

Maafisa Afya kutoka Halmashauri ya wilaya Masasi wamefika Radio fadhila na kutoa elimu ya Mfumo wa MMAMA kwa namna unavyofanya kazi na mafanikio yaliyotokana na mfumo huo.

Ifahamike Mmama ni mfumo wa usafirishaji wagonjwa ulioboresha na unaowagusa moja kwa moja wagonjwa wa aina mbili wa kwanza ni Mama aliyejifungua ndani ya siku 42 na mtoto mchanga ndani ya siku 28 mfumo unahusika na usafirishaji.

Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mmama imefika kila kituo cha Afya na toka kuanza kwake mwaka 2023 mpaka sasa imewafikia zaidi ya akina mama 656.