kauli mbiu siku ya lishe Duniani yatekelezwa kwa vitendo
1 November 2024, 6:14 PM
Kwa mwaka , 2024, Mandhari ya Wiki ya Lishe ya Kitaifa kauli mbiu ni ” Lishe Bora kwa Kila Mtu “. Kaulimbiu hii inaweka lengo la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya maendeleo endelevu, ikisisitiza kukuza mlo unaokidhi mahitaji ya lishe ya watu binafsi katika hatua mbalimbali za maisha
Na katika kuadhimisha siku hii ya lishe Duniani kwa upande wa wilayani Masasi Elimu mbali mbali zilitolewa ikiwemo kutumia makundi saba ya vyakula lishe kwa usahihi,
pamoja na kutoa Elimu hii ya lishe bora kulikuwa na chakula cha mchana katika shule maalumu ya Lulindi ambapo mlo huo ulihusisha makundi saba ya vyakula ikiwa ni kusherehekea pamoja na kuotoa elimu
Sa mbamba na hayo pia ilisisitizwa kwa mama mjamzito kuanza cliniki kwa wakati na kutambua dalili za hatari kwa mama mjamzito.