Mafrateli 29 wapewa daraja takatifu la ushemasi
22 October 2024, 12:28 PM
Na Lawrence Kessy.
Mwenyezi Mungu ndiye anayeita na anapoita hakuna binadamu ambaye anazuia hata kama kuna mtu anasimamisha kwa kipindi fulani na yule anayeitwa anaitwa ili alitumikie Taifa la Mungu.
Hayo yamesemwa na Mhashamu Askofu Hendry Mchamungu ambaye ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam kwenye Adhimisho la Ibada ya Misa Takatifu ya Daraja Takatifu la Ushemasi kwa Mafrateri 29 iliyofanyika katika Kanisa la Bikira Maria Mama wa Mungu, lililopo Chuoni Kikuu cha Jordani Morogoro, Jimboni Morogoro.
Amesema kwamba Shemasi anayo majukumu ya huduma kama kubatiza, kushuhudia ndoa kama hamna Padre, kuzika, kumpelekea mgonjwa anayekufa Komunyo Pamba na siyo kuungamisha au kutoa Mpako Mtakatifu wala kuadhimisha Misa na kuwataka wawe makini katika kutoa majukumu yao na kuwaomba kufanya kwa bidii.
Tena nyinyi nyote ni Watawa! Achaneni na mambo ya ulimwengu huu na mkiwahudumia watu vizuri nao watakaa nanyi vizuri na ndiyo watakaowatunza, hivyo nawaomba mchape kazi na ninawaombea siku moja mfikie Upadre mpate kuhudumia Kanisa la Mungu. Alesema askofu Hendry Mchamungu