Radio Fadhila

Mbunge Masasi awafikia wafanyabiasha walioathiriwa na kuungua kwa soko

4 August 2024, 9:23 PM

Mbunge wa Jimbo la Masasi Mji Geoffrey Mwambe ameendelea na ziara yake katika kata ya Mkuti na kufanikiwa kuzungumza na wananchi waliofika eneo hilo.

Akizungumza na wananchi Mhe Mb.Mwambe amesema wafanyabiashara waliopata maafa ya moto sokoni Mkuti ambao walikopa katika Banki ya CRDB,NMB,NBC baada ya kufanya kikao na Mameneja wa banki hizo wamefikia kutowadai pesa wafanya biashara hao badala yake pesa waliyokatwa wakati wanachukua mkopo kama Bima itumike kufidia.

Ziara hio ilihudhuriwa na Pia na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Ndg. Reuben Sixbert Jichabu, Viongozi wa Serikali, Vyama vya Siasa na wananchi kutoka maeneo tofauti tofauti .