Radio Fadhila

Baraza la madiwani lapokea na kujadili taarifa za kata

3 May 2024, 7:42 PM

Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Masasi chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Hashim Namtumba April 30, 2024 limepokea, kujadili na kupitisha taarifa za kata robo ya tatu, 2023/2024 katika mkutano wa Baraza la Madiwani

Baraza hilo limepokea, kujadili na kupitisha Taarifa za kata ya Chanikanguo, Jida, Migongo, Mkomaindo, Mkuti, Temeke, Mumbaka, MwengeMtapika, Napupa, Nyasa, Sululu, Mtandi, Marika na Matawale.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa Baraza hilo, waheshimiwa madiwani wameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji Masasi.

wamezungumza kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji, umeme, elimu na miundombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali ya Mji.

Aidha, limempongeza Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini Mhe. Geoffrey Mwambe kwa jitihada zake za kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo unawafikia wananchi wa Kata zote 14 za Halmashauri ya Mji Masasi.

Baraza hilo, limempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Ndg. Reuben Sixbert Jichabu kwa kasi yake ya kusimamia vyema na kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati, ufanisi, ubora na kutumika kwa wakati.