Radio Fadhila

Jela miaka 30 aliyemlaghai mtoto kwa njiwa na simbilisi

1 May 2024, 12:08 PM

Na Lilian Martin.

Masasi.

Ndugu Habibu Yahya Waziri mkazi wa Nyasa Masasi mwanye umri wa miaka 22 amehukumiwa kifungo Cha miaka 39 jela Kwa kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 10 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la Tano jina limehifadhiwa .

Kwa mujibu wa mashahidi wa kesi hiyo walisema kuwa Habibu Yahya alimlaghai mtoto huyo Kwa kumuambia aendenaye nyumbani kwake akaangalie Njiwa na Simbilisi ambao anawafuga.

mtoto huyo aliongozana na Habibu na walipofika nyumbani alimlazimisha kuvua nguo na kumtendea tukio hilo

na kutokana na ushahidi uliotolewa mahakama ilimtia hatiani ndg Habibu Yahya na kumuhukumu kifungo Cha miaka 30 Kwa kosa la kulawiti.