Shirika la SDA lagawa vifaa vya michezo shule za msingi, sekondari Masasi
29 May 2023, 9:32 AM
MASASI.
Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na michezo Sports Development Aid SDA, limeunga mkono juhudu za serikali za kuhakikisha jamii inajengewa uwezo wa kuwa na afya njema kwa kugawa vifaa vya michezo kwa shule za msingi na sekondari za halmsahuri ya mji wa Masasi na halmashauri za wilaya zipatazo 11.
Afisa Utumishi Halmashauri ya Mji wa Masasi Jumanne Chaula kwa niaba ya Mkurugenzi, akipokea Vifaa vya Michezo kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la DSA, Esta Vincent Sondoka.
Vifaa hivyo vya michezo vilivyotolewa ni pamoja na jezi, mipira, na vingine vinatajwa kuwa na thamani ya shilingi zaidi ya milioni kumi ikiwa ni sehemu ya mradi wake wa kuwawezesha watoto wa kike kupaza sauti unaotekelezwa ndani ya wilaya hiyo ya Masasi.
Akizungumza katika kutoa shukrani zake kwa shirika hilo afisa utumishi Jumanne Ibrahim Chaula, akikaimu nafasi ya mkurugenzi wa mji wa Masasi Elisi Ntilihungwa, akatumia nafasi hiyo kuzitaka taasisi zingine kuiga mfano huo kwa kusema…
Kwa upande wake Afisa Elimu wa shule za sekondari kutoka halmashauri hiyo Elentruda Mtevele, akizungumza kwa niaba ya afisa michezo wa halmashauri hiyo akatumia nafasi hiyo kuwaasa walimu kutunza vifaa hivyo kwa kusema
Wanafunzi na walimu wakizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo …voxpop..
Naye mratibu wa msaada huo Esta Vicent Sondoka akizungumza mara baada ya kugawa vifaa hivyo vya micheo akatumia nafasi hiyo kutoa shukrani zake kwa serikali kwa kusema
Ikumbukwe Miongoni mwa shule ambazo zimenufaika na msaada huo ni pamoja na shule ya msingi Masasi Maalum na Mtandi Maalum.