Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoa wa mtwara yafanyika wilayani masasi!
8 March 2021, 4:01 PM
Maadhimisho ya siku ya wanawake dunia ambayo huazimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 8 mwezi wa 3 yamefikiwa kilele chake hii leo , maadhimisho hayo. katika mkoa wa mtwara yamiadhishwa katika wilaya ya msasasi uwanja wa boma na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa mkoa na wilaya , mkuu wa wilaya ya msasi mh. seleman mzee na mgeni rasmi katika sherehe hizo alikuwa ni mkuu wa mkoa wa mtwara mh MH GELASIUS BYAKANWA ya kiwa yamebeba kauli mbiu isemayo MWANAMKE KATIKA UONGOZI CHACHU YA KUFIKIA DUNIA YENYE USAWA
Maadhimisho hayo yalienda sambamba na maandamano ya kinamama yakiwa na mabango yaliyobeba jumbe tofauti tofauti kuelekea uwanja wa boma , baadhi ya wajasilia mali wanawake na vikundi mbalimbali walileta bidhaa zao na kuziuzi katika maadhimisho hayo .
Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa mtwara mh gelasius byakanwa aliwapongeza wanawake kwa kazi mbalimbali walizo zifanya katika kipindi chote cha week katika kuelekea maadhimisho haya ya siku ya mwanamke duniani
Pia mkuu wa mkoa wa alisema wanawake wanayo nafasi ya kushiriki katika ukombozi wa jamii hii kama vile alivyopatikana makamo wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania samia suruhu, naibu spika wa bunge, waziri wa afya ,pia wa kuu wa mikoa wanawake pamoja na wakuu wa wilaya kama mkuu wa wilaya ya newala
Ikumbukwe tu maadhimisho haya ya Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa tarehe 8 Machi ya kila mwaka. Siku hiyo ilianza kuadhimishwa tarehe 8 Machi 1975 baada ya Umoja wa Mataifa kuridhia siku hii kutumika kama siku rasmi ya kuikumbusha dunia juu ya haki za wanawake.