KIUNGO wa Yanga, Carlos anasikitika kwa kuonyeshwa kadi nyekundu
28 February 2021, 4:07 AM
KIUNGO wa Yanga, Carlos Carlinhos amesema kuwa anasikitika kwa kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora uliochezwa Uwanja wa Uhuru.
Jana, Februari 27 wakati Yanga ikishinda bao 1-0 dhidi ya Ken Gold FC ya Mbeya, Carlinhos alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 80.
Aliingia uwanjani dakika ya 66 na alikutana na adhabu hiyo baada ya kumpiga ngumi ya chemba beki wa Ken Gold, Boniface Mwanjonde.
Nyota huyo raia wa Angola amesema kuwa anasikitika kwa alichokifanya kwa kuwa hakutarajia jambo ambalo linampa presha.
“Ninasikitika kwa kadi nyekundu ambayo nimepata hivyo sina la kusema zaidi ya kuomba msamaha kwa kile ambacho kimetokea,”.
Kwa upande wake beki Mwanjonde amesema kuwa alikutana na ngumi hiyo ya mbavu baada ya kumziba njia raia huyo wa Angola.
“Ilikuwa ni ngumi ya mbavu baada ya kumzidi spidi yeye alikuja mwilini hapo niliweza kumziba njia na mpira ulitoka nje.
“Wakati tunarudi uwanjani akaja akanipiga ngumi ya mbavu ila niliskia maumivu sio kivile kwa kuwa niliweza kurejea na kuendelea na mchezo,”.
Kwenye mchezo huo ambao umeipa Yanga tiketi ya kusonga hatua ya 16 bora bao lilifungwa na Fiston Razack dakika ya 40 kwa mkwaju wa penalti