Tatizo la kupata Hedhi nyingi kupita kiasi sababu na athari zake
Tatizo la kupata Hedhi nyingi kupita kiasi sababu na athari zake
31 December 2020, 4:03 AM
Kupata hedhi kupita kiasi ni moja ya matatizo ya uzazi yanayosumbua wanawake wengi. Tafiti zimeonyesha kwa kila wanawake 1000; wanawake 53 kati ya huwa na tatizo la kupata hedhi kupita kiasi. Ni theruthi tu ya wanawake wenye shida ya hedhi hutafuta tiba stahiki kwa daktari wengi hukaa nayo kwa aibu au hofu.
Makala hii nimegusia katika lugha rahisi visababishi vya hedhi kutoka nyingi ili itoe mwanga kwa wanawake kutafuta tiba pale wanapokabiriwa na changamoto hii
Je ni wakati gani mwanamke anatakiwa kuhisi kuwa anapata hedhi kupita kiasi?
Unapata hedhi inayozidi siku 7
Unapata hedhi nzito inayofanya ubadiri pedi moja ndani ya masaa mawili
Unapata hedhi nzito inayokulazimu kuvaa pedi zaidi ya moja
Sababu gani huweza kuchangia mwanamke kupata hedhi nzito kupita kiasi?
Vivimbe kwenye kuta za mji wa kizazi; vivimbe hivi sio saratani huitwa fibroids
Yai kupevuka bila mpangilio (Irregular ovulation) ; hali hii husababisha kuta za mji wa mimba zivimbe na kuwa nene hivyo kutoa damu nyingi. Hutokea zaidi kipindi cha kuvunja ungo na kipindi cha kukaribia ukomo wa hedhi
Matatizo ya kugandisha damu
Matumizi ya dawa za kuzuia damu kuganda
Baadhi ya wanawake waliotumia vitanzi (IUD) hasa ndani ya mwaka wa kwanza
Maambukizi ya mji wa mimba na mirija ya uzazi (PID)
Endometriosis
Saratani ya mji wa kizazi; kwa kinamama waliofikia umri wa ukomo wa hedhi. Wakianza kupata hedhi isiyokoma huweza kuwa dalili ya ya saratani ya mji wa kizazi
ATHARI ZA HEDHI NZITO KUPITA KIASI KWENYE AFYA
Hedhi nzito kupita kiasi huchangia wanawake wengi kupata upungufu wa damu
Hedhi kuwa nzito kupita kiasi huweza kuwa ni dalili ambao unahitaji tiba ya haraka
Huweza kuchangia kudhoofisha afya ya akili ya mwanamke ikiwemo kujiamini na wasiwasi
Nini hufanyika unapomuona daktari kuhusu tatizo la kupata hedhi kupita kiasi ?
Unapomuona daktari atachukua historia ya afya yako kwa ujumla
Historia ya afya ya uzazi na mzunguko wako wa hedhi
Historia ya dawa zote unazotumia
Daktari atahitaji kukufanyia vipimo vya mwili ili kuangalia kama kuna kisababishi kinachochangia hedhi kutoka kwa wingi
Daktari naweza chukua damu kupima wingi wako wa damu , kiwango chako cha homoni za uzazi pia na vipimo vingine kulingana na alivyokuona
Datari anaweza kukufanyia ultrasound ili kungalia mji wa uzazi na via nyingine za uzazi kama kuna tatizo
Je ni tiba aina gani hutumika kutibu tatizo la kupata hedhi nyingi kupita kiasi?
Tatizo la kupata hedhi nyingi kupita kiasi hutibiwa kulingana na chanzo kilichosababisha tatizo hilo, afya yako kwa ujumla na uchaguzi wako tiba; baadhi ya tiba ni pamoja na :
Tiba ya dawa zenye homoni
Tiba za dawa za kugandisha damu — Hutolewa iwapo hedhi inayotoka ni nyingi sana
Upasuaji wa kuondoa vivimbe vya fibroids
Tiba ya kukwangua kuta za mji wa mimba
Tiba ya kuziba mishipa ya damu ya mji wa kizazi. Huitwa “uterine artery embolization”