TAEEs yatoa mafunzo kwa bodi za maji 15 Mufindi
21 September 2023, 18:46
Na Kelvin Mickdady -MufindiFM
Bodi za kusimamia vyanzo na usafi wa maji wilayani Mufindi zimetakiwa kuboresha mfumo wa ufanyaji kazi ili kuongeza mapato ya serikali kupitia bodi hizo.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya Mufindi Mhe. Festo Mgina wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo vyombo vya watoa huduma ya maji na kusema kuwa inatakiwa kuwe na ushirikiano kati ya viongozi wa bodi na jamii.
Sanjari na hayo Mhamasishaji mradi wa shirika la wahandisi Mazingira Tanzania Bi. Sayun Mbiga amesema kuwa mafunzo hayo yanakwenda kuongeza ufanisi katika utendaji kazi kwenye bodi za maji.
Kwa upande wake Afisa maendeleo Kutoka Wakala wa Maji na Usalama wa Mazingira Vijijini RUWASA Josephat Kyando ameitaka jamii kulipia maji ili kuongeza mapato.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa elimu hiyo waliyoipata inakwenda kubadili mfumo wao wa utendaji kazi.
Mafunzo ya kuwajengea uwezo vyombo vya watoa huduma ya maji Ngazi ya jamii (CBWS) Yamefunguliwa Sept 20 Na kutamatika leo Septemba 21/09 Kwa halmashauri ya wilaya ya Mufindi.