

21 February 2025, 07:10
na Jumane Bulali
Mufindi FM Radio 107.3 imeshika nafasi ya tatu Kwa kulipa Kodi Kwa wakati na kwa usahihi Kwa upande wa Vyombo vya Habari vya Mkoa wa Iringa.
Mufindi FM imepewa tunzo hiyo maalumu baada ya kutambuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Iringa wakati wa usiku wa Utolewaji wa Tuzo kwa walipa Kodi wa nyaja mbalimbali.
Akizungumza wakati wa Utolewaji wa Tuzo hizo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Peter Serukamba mbali na kuwapongeza Washindi mbalimbali pia ametoa wito Kwa Wafanyabiashara kulipa Kodi kwa hiyari.