Mufindi FM

Kikundi cha Mkombozi kuinuka kiuchumi

26 November 2024, 06:25

Mlezi Wa Kikundi cha Mkombozi Ndugu Fredric Kalinga akipokea Risala ya kikundi hicho.

Na Kefa Sika

MUFINDI

Kikundi cha Mkombozi kilichopo katika kijiji cha Kidete kata ya Mdabulo wilayani Mufindi Mkoani Iringa chenye wanachama 61 kimepokea fedha kiasi Cha shillingi laki 5, Kwa ajili ya Uendeshaji wa kikundi hicho.

Kikundi hicho hujishughulisha na ufugaji ili kujiletea maendeleo na kujikwamua kiuchumi.

Kiasi hicho Cha Pesa kimetolewa na mdau wa maendeleo wilayani Mufindi ambaye pia ni meneja wa mawasiliano na masoko wa wakala wa majengo Tanzania TBA Ndugu Fredric Victory Kalinga ambaye pia ameteuliwa kuwa mlezi wa kikundi hicho na kuahidi kuendelea kushirikiana na wanakikundi .

Sauti ya Fredrick Kalinga

Nao baadhi ya wanakikundi hicho wamemshukuru Ndugu Fredrick Kalinga kwa kuwasaidia kwenye namna bora ya kukiinua kikundi hicho.

Sauti ya Wanakikundi wa Mkombozi

Mwisho