Mwenge wa Uhuru kuzindua miradi yenye thamani zaidi ya Bilioni 600 Iringa
21 June 2024, 14:11
Na Moses Mbwambo
Iringa
Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuwasili mkoani Iringa Juni 22,2024 ukitokea mkoani Njombe ambapo utazinduaa miradi yenye thamani ya zaidi ya bilioni 600 na utakimbizwa kwenye Halmashauri 5 za mkoa wa Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba Juni21,2024 amewaambia wanahabari kuwa Mwenge huo utapokelwa mkoani humo ukitokea Mkoani Njombe ambapo mapokezi yatafanyika kwenye Kijiji cha Nyigo wilaya ya Mufindi na utakagua na kuweka mawe ya msingi miradi 50.
Ambapo Mhe. serukamba amesema kwamba mwenge huo unatarajiwa kukimbizwa umbali wa kilomita 873.03 na baada ya kumaliza mbio zake mkoani hapa utakabidhiwa mkoani Dodoma
.Aidha Mhe. Serukamba amewataka wananchi wote mkoani hapa kujitokeza kwa wingi kuupokea na kuulaki mwenge wa uhuru katika mapokezi,barabarani,kwenye miradi na maeneo ya mikesha.
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru wa Mwaka 2024 inasema “Tunza Mazingira, na shiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa ujenzi wa taifa Endelevu”