Mufindi FM

Vijana 192 kupata ajira Sao Hill

21 June 2024, 11:34

Mmoja kati ya vijana akifanyiwa usaili kwa kusaidia kusaidia kupambana na majanga ya moto na jopo la viongozi wa shamba la miti Sao Hill. Picha na Kefa Sika.

Na Kefa Sika

Mafinga

Takribani vijana 192 wanatarajia kupata ajira za ulinzi wa misitu dhidi ya majanga ya moto shamba la miti saohill lenye ukubwa wa hekta 134,903 wilayani Mufindi kuanzia julai Mosi Mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Msaidizi wa Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Saohill Bw. Said Singano akizungumza katika zoezi la usahili wa vijana wanaochaguliwa kujiunga na kikosi cha kupambana na kuzuia majanga ya moto kwenye msitu huo.

Sambamba na hilo Bw. Singano ametoa wito kwa wananchi wanaolizunguka shamba kuendelea kuhakikisha wanafata taratibu zilizowekwa za uanzishwaji wa moto ili kuepusha moto usiotarajiwa.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha ulinzi wa msitu katika Shamba la Miti Saohill Murya Sawa amesema kuwa zoezi la kukabiliana na majanga ya moto katika misitu ni jukumu la kila mwanachi hivyo linahitaji uzalendo na ukakamavu.

Nao baadhi ya washiriki wa zoezi hilo wamesema kuwa wanaendelea kupambana na uanzishwaji wa moto kwenye msitu huo kwani kumekuwa na matukio mengi ya moto hasa msimu huu wa kiangazi.

Zoezi la usaili wa vijana wa kupambana na majanga ya moto limezinduliwa katika makao makuu ya Shamba hilo kwenye kijiji cha Ihefu na linatarajiwa kuendelea katika vituo vyote vya tarafa zote za Shamba tarafa ya kwanza Irundi, tarafa ya tatu Ihalimba pamoja na tarafa ya nne Mgololo.