Mufindi FM

Kuna hatari gani kulala na petroli au gesi?

30 September 2023, 20:01

Mfano wa chumba Cha kulala chenye mlundikano wa vitu ikiwemo nishati ya gesi ya kupikia.

Na Marko Msafili/Mafinga

Jamii imeaswa kuacha tabia ya kulala na Viminika ikiwemo mafuta au Vitu vinavyotumia nishati hiyo pamoja na kutambua namna sahihi ya kusimamia katika maeneo wanayoishi.
Rai hiyo imetolewa na Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilayani Mufindi Kamanda Kipunde Mgweno wakati akizungumza na Mufindi Fm 107.3 na kwamba kitendo hicho ni kinyume cha sheria na kinahatarisha Usalama wa raia.

Sauti ya Kamanda Kipunde Mgweno

Aidha Kamanda Mgweno amesisitiza uhifadhi sahihi wa vimiminika hivyo kwa Wafanyabiashara waishio maeneo ya vijijini huku akiwasihi kufuata sheria na utaratibu unaotolewa.

Sauti ya Kamanda Kipunde Mgweno

Sambamba na hayo Kamanda Kipunda amewasihi wananchi kuchukua tahadhari ya moto huku akiwataka kutumia namba ya dharura ya Jeshi la polisi la Zimamoto na Uokoaji ya 114 kutoa taarifa pindi yanapotokea maafa na majanga ya moto.