Vyama vya ushirika mwarobaini wa masoko kwa wakulima
30 September 2023, 19:30
Na Isaya Kigodi/Mafinga
Ili kuendana na mahitaji ya soko, Wakulima wilayani Mufindi wametakiwa kujiunga na vyama vya ushirika jambo ambalo litawarahisishia kulifikia soko.
Hayo yamesemwa na Afisa ushirika Halmashauri ya wilaya ya Mufindi Bi. Pili Mwaipaja wakati akizungumza na Mufindi Fm na kusema kuwa kigezo kikubwa ili kuunda chama cha ushirika ni kuwa na idadi ya wananchama wapatao ishirini.
Sanjari na hayo Bi. Mwaipaja amesema kwa watu wenye uhitaji wa kufungua chama cha ushirika wanatakiwa kuwa ni kikundi wanaofanya shughuli moja kama wakulima au wafugaji.
Mpaka kufikia mwishoni mwaka 2022 mkoa wa Iringa ulikuwa na vyama vya ushirika 47 ambavyo ni muungano wa AMCOS na SACCOS na miongoni mwa vyama vya ushirika vilivyopo wilayani Mufindi ni pamoja na Mbalamaziwa SACCOSna Sawala Women AMCOS Limited.