Kalinga: Wanafunzi 5 wasiojiweza kushikwa mkono
30 September 2023, 18:59
Na Gift Mario/Mufindi
Kaimu Meneja mawasiliano na masoko TBA Ndugu Fredrick Kalinga, amechangia mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa matundu 14 ya vyoo katika shule ya msingi Igulusi kata ya Ifwagi wilayani Mufindi.
Katika hotuba yake iliyowasilishwa na Ndugu Thomas Naftery Mtilega kwa niaba ya ndg. Kalinga ambaye ni Mgeni Rasmi kwenye mahafari ya darasa la saba mwaka 2023 shuleni hapo pia amechangia katoni 2 za chaki na kuahidi nkuwasaidia watoto watano wasiojiweza.
Naye kaimu Afisa Elimu kata Ndugu Niko Ngumbi akizungumza kwa niaba ya afisa elimu kata amewataka wazazi wa wahitimu kuwapeleka watoto sekondari ifikapo tarehe 02/10/2023.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Itona Ndugu Victambiasi Msigala amewashukuru wananchi kwa namna walivyo shirikiana kuhakikisha wanajenga choo cha wanafunzi kwa kushirikiana na serikali.
Awali serikali ilitoa kiasi cha shilingi Mil 38,258,000 kwa ajili ya mradi huo ikiwa hadi sasa umefikia 95% ambapo imesalia kuingiza maji na kufunika matundu lakini kupitia mahafari hayo wamefanikiwa kupata pesa kwaajiri ya kufunika matundu hayo.