Ileje FM

Kamishna Jeshi la Zimamoto Tanzania atoa cheti cha pongezi Ileje FM

September 30, 2025, 8:08 am

Mhariri Mkuu Ileje FM Denis Sinkonde kwaniaba ya meneja wa kituo hicho akipokea cheti cha Pongezi kutoka kwa kamishina wa jeshi la zimamoto mkoa wa Songwe Elautery Mremi.(Picha Pitison Mbughi).

Na Denis Sinkonde,Ileje

Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto Tanzania CGF John William Masunga amekabidhi cheti cha pongezi kwa redio ya jamii Ileje FM iliyopo wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe kwa utoaji elimu kwa umma kuhusu majanga ya moto na uokozi.

Cheti hicho kimekabidhiwa na kaimu kamishina wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Songwe Elautery Mremi kwaniaba ya kamishina wa jeshi hilo Tanzania John Masunga mbele ya watumishi wa kituo hiki katika ofisi za redio Ileje zilizopo Itumba.

Mremi amesema Ileje Fm ni miongoni mwa redio Tanzani na mkoa wa Songwe kukabidhiwa cheti kutokana na umahiri wake wa kutoa elimu ya majanga kwa kushirikiana na watumishi wa jeshi hilo mkoani Songwe.

Sauti ya kamishina wa jeshi la zimamoto mkoa wa Songwe

Mremi amesema kwa mkoa wa Songwe Ileje Fm imekuwa ikifanya vizuri kutoa elimu mbalimbali kwa umma kwa kualika wataalamu mbalimbali ikiwepo jeshi la zimamoto kutoa elimu.

“kwa hivi sasa kuna matumizi mengi ya nishati ya kupikia vijijini hivyo elimu inahitajika kwa wananchi namna ya kukabiliana na majanga yanoweza kutokea pindi watakapokuwa wanatumia gesi kupikia,”amesema Mremi.