Ileje FM
Ileje FM
September 26, 2025, 7:32 am

Na Denis Sinkonde
Songwe.Wafanyabiasahara na wananchi Mkoani Songwe wameaswa kuacha vitendo vya kukwepa ulipaji kodi kupitia Mamlaka ya Mapato mkoani humo(TRA) huku wakikumbushwa kuwa kodi ni muhimu kwa maendeleo ya taifa na wananchi.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Jabiri Omari Makame aliyasema hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa Dawati Maalumu la Uwezeshaji Biashara la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa Mkoa wa Songwe, hafla ambayo imefanyika katika viwanja vya Mlowo, wilayani Mbozi, na kuhudhuriwa na wajasiriamali, wadau wa benki, pamoja na wananchi wengine.
Makame aliwataka wafanyabiashara wote, hususan wajasiriamali wadogo na wa kati, kutambua kuwa kodi ni sehemu muhimu ya kuchangia maendeleo ya taifa huku akiwashauri kutumia huduma zinazotolewa na TRA kupitia Dawati hilo, ili kufahamu vizuri haki na wajibu wao kama walipakodi.
Kwa Mkoa wa Songwe ukusanyaji wa mapato kupitia Mamlaka ya mapato Tanzania TRA umeongezeka kutoka Sh 118 bilioni kwa mwaka 2021 mpaka bilioni 240.1 bilioni mwaka 2024-2025 ambapo kitaifa imeongezeka kutoka Sh 21.92 trioni mwaka 2021 mpaka Sh 31.64 trioni mpaka sasa.
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Songwe Jabir Omary Makame
“Ongezeko hilo la ukusanyaji wa kodi umetokana na mifumo dhabiti iliyowekwa na TRA kuwa rafiki kwa wafanyabiashara na wananchi kuwa na utayari wa kulipa kodi kwa hiari kwa maendeleo kwa mstakabali wa taifa,” amesema Makame.
Makame amesema ongezeko hili la mapato kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ni muhimu kwa ustawi wa taifa letu na ukuaji wa biashara zetu wenyewe na kutumia huduma bora kutoka TRA ili tusikie vizuri elimu ya kodi na kuondoa vikwazo,” amesema Makame.