Ileje FM
Ileje FM
September 10, 2025, 6:17 am

Na Denis sinkonde na Anord Kimbulu
Jumla ya watahiniwa 2641 wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi wilayani Ileje Mkoani Songwe utakaofanyika Septemba 10 na 11 mwaka huu.
Akizungumza na Ileje Fm juu ya maandalizi ya mitihani hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ileje Nuru Kindamba amesema tayari maandalizi yamekamilika ambapo matarajio ya mwaka huu ni kuongeza kiwango cha ufaulu kufikia asilimia 85 kutoka ufaulu wa asilimia 81 ya mwaka 2024.
Kindamba amesema tumefanikiwa kupandisha kiwango cha ufaulu kwa matokeo ya darasa la saba kuanzia mwaka 2023 ambapo wanafunzi walifaulu kwa asilimia 65, mwaka 2024 asilimia 81 namatarajio ya mwaka huu ni kufikia asilimia 85
Sauti ya mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Ileje Nuru Kindamba
“Kwa kushirikiana na timya ya wataalamu wa elimu wakiwemo walimu tumefanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha ufaulu unaongezea kwani hata mimi nilikuwa naenda kufundisha darasa kuangalia uwezo wa wanafunzi hivyo tutafanya vizuri,” amesema Kindamba.

Aidha Kindamba ametoa wito kwa wasimamizi kuzingatia maadili ya usimamizi wa mitihani huku akiwaonya wanafunzi kujiepusha na kuandika matusi.
Sauti ya Mkurugenzi wa Ileje Nuru Kindamba
“Niwasihi wanawafunzi kuzingatia mliyofundishwa darasani kwa kujibu maswali kwa utulivu huku wasimamizi wa mitihani mjiepushe na kufanya udanganyifu kwa watahiniwa,” amesema Kindamba.