Ileje FM

Sh 2.9 bilioni kujenga daraja Momba

June 10, 2025, 3:06 pm

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo aliyevaa kofia nyeusi ameambatana na mkuu wa wilaya Momba Elius Mwandobo wakati wa ukaguzi ujenzi wa daraja la Msangano-Chindi.Picha na Denis Sinkonde

Imeelezwa kuwa daraja hilo pindi litakapokamilika litawasidia wananchi wa halmashauri ya Momba na Tunduma kurahisisha shughuli za usafirishaji yakiwepo mazao.

Na: Denis Sinkonde

Momba.Serikali imeanza ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 54 linalounganisha halamashauri ya Momba na Tunduma wilaya ya Momba Mkoa wa Songwe kwa linalojengwa kwa gharama ya Sh 2.9 bilioni.

Hayo yamebainishwa na mkuu Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo wakati akifanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika halmashauri ya Momba ukiwepo mradi wa ujenzi wa daraja la Msangano- Chindi huku akisema ujenzi wa daraja hilo utakapokamilika utawarahisishia mawasiliano wananchi wa halmashauri hizo mbili amabo wanajihusisha na kilimo cha mpunga, mahindi na ufuta.

Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa daraja hilo Meneja wa Wakala wa Barabara (TARURA) wilaya ya Momba Yusuph Shaban amesema daraja hilo litajengwa kwa thamani ya Sh 2.9  bilioni lina urefu wa mita 54.

Shabani amesema ujenzi huo unatarajia kukamilika ndani ya miezi 24, ambapo hadi sasa limekamilika kwa asilimia 65 baada ya miezi 19 ya utekelezaji, na miezi 5 imebaki kukamilisha mradi na hadi kufikia sasa, mkandarasi amelipwa Shilingi Bilioni 1.5.

Sauti ya meneja wa Tarura wilaya ya Momba………………………………………

“Daraja hilo linatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika ifikapo Oktoba 2025, na litakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Tarafa ya Msangano na Wilaya nzima ya Momba, kwa kuwa litaboresha mawasiliano na kurahisisha usafiri kati ya Momba na Tunduma,” amesema Shabani.

Mkuu wa wilaya ya Momba Elius Mwandobo amesema daraja hilo ni kiunganishi kikubwa cha makao makuu ya wilaya ya Momba yaliyopo Chitete na Halmashauri ya Tunduma  hivyo litakapokamilika ltasaidia kukuza uchumi kwa wananchi wa wilaya ya Momba katika masuala ya kilimo na usafirishaji.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Momba

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa daraja hilo Mkuu wa Mkoa huo Daniel Chongolo amempongeza mkandarasi kwa juhudi na kasi nzuri ya utekelezaji wa mradi huo kwani awali alipofika kukagua ujenzi huo alikuta mradi upo asilimia 5 na sasa umefika asilimia 65.

 Amesema kuwa kwa muda mrefu kusafiri kutoka Tunduma kupita eneo hilo ilikuwa ni anasa, lakini kukamilika kwa daraja hilo kutamaliza changamoto hiyo kwa wananchi wa Msangano na maeneo yote ya Momba.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Songwe

eneo la daraja linalojengwa katika halmashauri ya Momba ambalo linaunganisha halmashauri mbili za Momba na Tunduma Mkoani Songwe.Picha na Denis Sinkonde

Faraja Sikapizye mkazi wa Msangano wilayani Momba amesema daraja likikamilika litakuwa ni mkombozi kwa halmashauri ya Momba kwani kizuizi kikubwa ilikuwa ni kukosekana kwa daraja.

Sauti ya mwananchi