Ileje FM

Udumavu bado tatizo Ileje

June 5, 2025, 7:10 am

Mkuu wa wilaya ya Ileje akiwa na watoto wa kitongoji cha Nkanka kijiji cha Itumba katika siku ya afya na lishe. picha na Sikudhani Minga

Asilimia 40 ya watoto wa kitongoji cha Nkaka kijiji cha Itumba wanakabiliwa na udumavu.

Na:Sikudhani Minga

Halmashauri ya wilaya ya Ileje Mkoani Songwe inakabiliwa na changamoto za udumavu kwa watoto luicha ya wananchi kuzalisha mazao mbalibali ya vyakula pamoja na ufugaji.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi Juni 4, 2025, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya kijiji, sambamba na kampeni ya utoaji wa vitamini A na dawa za minyoo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, iliyofanyika katika kitongoji hicho.

Mgomi, ametoa wito kwa wananchi wa kitongoji cha Nkanka kilichopo kijiji cha Itumba, Kata ya Itumba wilayani hapa, kuzingatia lishe bora kwa watoto ili kuwawezesha kuwa na afya bora na makuzi imara.

Akizungumza katika tukio hilo, Mgomi amesema kuwa lishe duni ni chanzo kikuu cha udumavu na matatizo ya ukuaji kwa watoto, hivyo jamii inapaswa kubadili mtazamo na kuhakikisha watoto wanapata chakula chenye virutubisho muhimu.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Ileje………………

Mgomi amesema katika kitongoji hicho asilimia 40 ya watoto wanaudumavu uliosababishwa na ukosefu wa lishe.

Sauti ya mkuu wa wilaya Ileje

“Kina baba wanapaswa kushiriki kikamilifu kuwapeleka watoto kliniki pamoja na kina mama, kwa ajili ya chanjo, huduma za lishe na ufuatiliaji wa afya hii itasaidia kujenga kizazi chenye afya njema na uwezo mkubwa wa kujifunza na kufanya kazi katika siku za usoni,” aamesema Mgomi.

wananchi wa kitongoji cha Nkanka wakiwa kwenye mkutano.picha na Sikudhani Minga

Ameeleza kuwa afya bora ya mtoto huanza nyumbani, na hivyo wazazi wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha watoto wao wanapata mlo kamili kila siku.