Habari za Jumla
January 29, 2023, 8:42 am
Watendaji wa Kata simamieni Wanafunzi waende Shule-Dc Sweda
Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda amesema kiwango cha wanafunzi Tarafa ya Ikuwo kuripoti shule ni hafifu Ameagiza Afisa Tarafa, watendaji wa kata kufanya msako maalumu kuhakikisha wanafunzi ambao hawajaripoti kidato cha kwanza mpaka sasa wanaripoti shule na…
January 29, 2023, 8:12 am
Tumieni Vishikwambi kwa manufaa ya Elimu- Mkurugenzi Makete
Mkurugenzi Mtendaji Halashauri ya Wilaya Makete William Makufwe amewataka walimu kutunza Vishikwambi walivyopewa na kuvitumia kwa lengo lililokusudiwa. Makufwe ametoa rai hiyo wakati wa makabidhiano ya Vishikwambi hivyo yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi huu Januari, 2023 Ameongeza kuwa kwa yeyote atakayebainika…
January 29, 2023, 8:02 am
Vifaa vya Huduma ya Dharura vimeunganishwa Hospitali ya Wilaya Makete
Zoezi la kufunga vifaa tiba vya kisasa jengo la dharura (EMD) Hospital ya Wilaya ya Makete Mkoa wa Njombe limefanywa na wataalamu kwa lengo la kuanza kutoa huduma za Afya Hospitalini hapo. Serikali imetoa Milioni 300 kujenga jengo hilo la…
January 29, 2023, 7:54 am
UWT Njombe wapanda miti Ilumaki Sekondari
Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Njombe wamefanya Maadhimisho ya miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi Wilayani Makete kwa kupanda miti kuzunguka eneo la shule ya Sekondari Ilumaki iliyopo Kata ya Lupalilo Wilaya ya Makete. Zoezi hilo limefanywa…
January 29, 2023, 7:43 am
Mfuko wa Jimbo Makete waongezeka kutoka Milioni 36 hadi Milioni 59
Serikali imeongeza mfuko wa Jimbo la Makete kutoka Milioni 36,282,000 kwa mwaka 2021/2022 hadi kufikia Milioni 59,647,000 kwa mwaka 2022/2023. Kupitia Kikao cha Baraza maalumu la Madiwani kilichofanyika leo Tarehe 27 Januari 2023 cha kupitisha Bajeti ya mwaka wa fedha…
January 27, 2023, 10:56 am
Nchi ya Haiti yaja Njombe kujifunza Mbinu za utoaji wa Chanjo ya Uvico 19
Serikali ya Hait toka Amerika ya kusini imetuma wajumbe wake kuja kujifunza katika wilaya ya Njombe namna ilivyofanikiwa katika utekelezaji wa utoaji wa Chanjo ya UVICO 19 kupitia kampeni maalum ya kijiji kwa kijiji chini ya mkuu wa Wilaya ya…
January 27, 2023, 7:55 am
Jamii ijikite kusuluhisha Migogoro-Mhe. Ivan Msaki
Hakimu mkazi mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Makete Mh. Ivan Msaki amesema jamii ikijikita katika utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi kutaifanya jamii yenyewe kuishi bila uhasama. Mh. Msaki ameyasema hayo januari 25,2023 wakati akizungumza na wanafunzi wa chuo…
January 27, 2023, 7:28 am
Wazazi wawajibike kulea Watoto-Mwanasheria Makete
Wananchi wametakiwa kuhakikisha wanahudumia Familia hususani watoto pale wazazi/wanandoa wanapokuwa wametengana kwa sababu mbalimbali. Rai hiyo imetolewa na Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Makete Ndg. Appolo Laizer akizungumza na Kitulo FM kwenye Kipindi cha Daladala tarehe 27…
January 25, 2023, 4:00 pm
MNEC Njombe ampongeza DC Makete kuaminiwa na Rais
Mwakilishi wa Mkutano Mkuu CCM Taifa Mkoa wa Njombe (MNEC) Ndg. Abraham Okoka amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda kwa kuaminiwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuwatumikia wananchi wa Makete MNEC ametoa pongezi hizo leo…
January 25, 2023, 2:19 pm
Miche elfu 20 ya Parachichi kugawiwa kwa Walengwa wa TASAF Makambako-Njombe
Ili kukabiliana na umasikini uliopo kwenye baadhi ya familia mkoani Njombe Serikali chini ya Wizara ya Kilimo imegawa miche elfu 20 kwa kaya zinazonufaika na mpango wa TASAF Katika Halmashauri ya mji wa Makambako. Akitoa miche hiyo katika kata ya…