Radio Fadhila

Familia ya aliyekuwa Muhimbili yahudumiwa na wasamaria wema

9 October 2024, 8:21 PM

Christine simo akiwa na familia

Na. Lilian Martin

Familia ya kijana anaye fahamika kwa jina la Bw. Issaya mkazi wa Masasi mtaa wa Nyasa ambaye kwa sasa yupo hospital Muhimbili kwa ajili ya matibabu imepokea msaada kutoka shirika lisilo la kiserikali la upendo charity.

Ikiwa moja ya kazi inayofanywa na shirika hilo ni kusaidia wenye uhitaji wamefanikiwa kumpeleka mgonywa huyo kupata matibabu muhimbili kwa mara kadha na sasa wamewafikia wanafamilia na kutoa msaada wa chakula.

Kwa niaba ya wanafamilia hao Bintu luca aliwashukuru Upendo charity kwa kuonyesha upendo mkubwa kwao.

Sina cha kuwalipa kwa wanachokifanya kwetu wao ndio waliompeleka Issaya Hospital na kufuatilia gharama zote za matibabu Mungu awabariki sana.Alisema Bintu luck

aliendelea na kusema kuwa kama mnavyoona issaya anaugua na hali ya maisha siyo nzuri na sasa familia yote tupo pamoja na watoto wake.