Radio Fadhila

Comrade Mobitu ajitambilisha kwa wanachama baada ya kuteuliwa

1 October 2024, 4:36 PM

MASASI.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Mtwara Comrade Mobutu Malima amefanya mkutano na Wajumbe wa Chama hicho kutoka Wilaya ya Masasi ikiwa ni sehemu ya kuja kijitambulisha Baada ya kuteuliwa kuwa Katibu wa Ccm Mkoa wa Mtwara.

Akizungumza na Wajumbe wa Sekretariet Masasi Comrade Mobutu Amewataka Makatibu wa kwenye vyama,Jumuiya,Kata pamoja na Matawi waweze kuitisha vikao vya Wajumbe kwani pasipo kufanya hivyo watakua wamekiuka Katiba kama inavyotaka.

Ameongeza kwa kusema “nisichaguliwe rafiki wala adui kwa pamoja wote ni ndugu zangu tushirikiane kukijenga Chama chetu pamoja na Kuijenga Nchi yetu kwa Pamoja na anayetaka kututikisa katika nchi yetu Tumuone ni Adui.

Mkutano huo umefanyika Wilayani Masasi katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya na kuhudhuriwa na Viongozi wa Chama, Wabunge wa Majimbo ya Masasi Mji na Ndanda, Wajumbe wa jimbo la Masasi Mji,Lulindi pamoja na Ndanda.