Radio Fadhila

Mbunge wa jimbo la Masasi akabidhi vifaa tiba kituo Cha afya mtandi

10 May 2024, 5:30 PM

Mbunge wa Jimbo la Masasi mjini,Geofrey Mwambe (CCM) ametoa vifaa tiba katika kituo cha Afya cha kata ya Mtandi halmashauri ya mji Masasi mkoani Mtwara ili kuweza kuhimarisha upatikanaji wa huduma bora ya afya kwa wananchi wa kata hiyo, vifaa hivyo vinathamani ya zaidi ya shilingi milioni 1.4.

Kwa niaba ya Mbunge,Geofrey Mwambe, katibu wa Mbunge,Rashidi Mpungula amekabidhi vifaa hivyo kwa Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Mtandi,ambapo alieleza kwamba kwa niaba ya Mbunge Mwambe kupitia ofisi ya Mbunge wametoa vifaa hivyo ili kuweza kuhimarisha huduma za afya kwa wananchi wake.

Amesema kuwa Mbunge Mwambe atahakikisha vifaa kama hivyo anavitoa katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya katika kila zahanati za vijiji na vituo vya Afya katika kila kata ziliozopo Jimbo hilo la Masasi mjini.

Kwa upande wake,Mganga Mfawidhi wa kituo hicho cha Afya cha kata ya Mtandi, Hajirati Mapembe amesema kuwa wanamshukuru Mbunge Mwambe kwa kuwapatia vifaa tiba hivyo na kwamba vimevika wakati mahususi kituo hicho kikikabiliwa na upungufu wa vifaa tiba.

Mganga Mfawidhi huyo amevitaja vifaa ambayo Mbunge Mwambe ametoa kwa kituo hicho cha afya kuwa ni vitanda 15 vya kulazia wagonjwa, vitanda 10 vya uchunguzi, magodoro 15 kabati 15 za kuhifadhia vifaa vya matibabu, meza saba kwa ajili ya wagonjwa kulea chakula wakiwa wodini na shuka za wagonjwa 60
Amesema vifaa hivyo vyote vimetolewa na Mbunge Mwambe kwa jitihada zake mwenyewe hivyo anapaswa kupongezwa kwa nguvu kubwa anayoitumia katika kuleta maendeleo chanya kwa ajili ya wananchi wa Jimbo la Masasi mjini