Radio Fadhila
Radio Fadhila
19/03/2026, 08:01

Kutokana na kuwepo kwa taarifa nyingi za upotoshaji katika mitandao ya kijamii Taasisi ya jamii Afrika imeona ipo sababu ya kutoa Elimu juu ya kutambua ukweli wa habari hizo ili kupunguza wimbi la taarifa potofu katika vyombo vya habari
Na: Lilian Martin
Taasisi ya Jamii Afrika inayojulikana kama Jamii Forum imetoa mafunzo maalum kwa wanahabari mkoani Mtwara, yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kutambua na kupambana na taarifa za upotoshaji katika mitandao ya kijamii.
Katika mafunzo hayo waandishi waliweza kutambua namna sahihi ya kuthibishisha taarifa na kupambana na wimbi la taarifa potofu katika Mitandao

Sambamba na hayo waandishi walipata nafasi ya kueleza juu ya kile walichofundishwa na namna kilivyo na tija katika kazi zao
kutokana na Mafunzo hayo waandishi wa habari wameishukuru taasisi ya jamii Afrika na kuahidi kutumia kalama zao vizuri kwa kuwapa wananchi taarifa bora na sahihi.
Na mmoja wa kukufunzi katika mafunzo hayo alisema kuwa “kutokana na matumizi na uhuru wa kutumia mitandao ya kijamii mtu afanya chochote mtandaoni na matumizi ya akili mnemba (AI)ni makubwa zaidi hivyo ni vyema waandishi kuwa makini zaidi”
