Radio Fadhila

Gari la abiria kichaka cha kusafirisha madawa ya kulevya

19 January 2026, 1:42 PM

Gari likilokamatwa na Madawa

Na Lilian Martin

Pamoja na muonekano wake wa nje kuonekana ni Gari la abiria ila kwa ndani kuna chemba ya maficho mizigo haramu ambayo kwa kawaida huwezi kubaini, ila wahenga husema za mwizi 40 na leo zimeshafika.

Katika Wailes, Temeke , Dar es Salaam, zilikamatwa pakiti 20 za skanka zenye uzito
wa kilogramu 20.03 zikiwa zimefichwa ndani ya balo la mitumba na kufichwa kwenye bus aina ya Scania la kampuni ya King Masai Tours, lenye namba za usajili wa nchi ya Msumbiji namba AAM 297 CA . Bus hilo hufanya safari zake kati ya Nampula nchini Msumbiji na Tanzania.
Watuhumiwa waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo ni Amasha Iddi Mrisho (40), mkazi wa Buza,
Dar es Salaam na Seleman Juma Ally (32), raia wa Msumbiji.

Ni chemba iliyopo ndani ya basi hilo

Ni mizigo ilivyokutwa ndani ya chema ya siri