Radio Fadhila
Radio Fadhila
14 June 2025, 3:24 PM

Mtafiti wa kilimo akitoa maelezo
Katika kuifikia adhima ya serikali ya kuongez uzalishaji wa zao la kotosho kwa mwaka 2025-2026 hadi kufikia tani millioni 1 kwa mwaka 2029-2030 maafsa ugani wapewa mafunzo yatakayoleta tija kwa wakulima
Na Lilian Martin
Maafsa ugani kutoka maeneo mbalimbali Wilayani Masasi wamepewa mafunzo juu ya matumizi sahihi na salama ya viwatilifu ili kuongeza uzalishaji wa zao la korosho na kufikia adhima ya serikali
katika mafunzo hayo yaliyotolewa na Taasisi ya Utafti na Kilimo Naliendele yamelenga kuwawezesha maafsa kupata elimu ili kuwasaidia wakulima wanao wahudumia katika maeneo wanayofanyia kazi
sambamba na hayo maafsa ugani wamezungumza juu ya changamoto wanazo kutana nazo katoka maeneo ya kazi ikiwa pamoja na mkulima kutumia viwatilifu kwa mazoea
na kwaupande wake Mtafiti kutoka Taasisi ya kilimo Naliendele walizungumzia juu ya matumizi salama ya viwatilifu pamoja na mashine zinazotuka katika upuliziaji
Na kwa upande wake Afsa kilimo mwandamizi kutoka bodi ya korosho Tanzania ambaye pia alizungumza juu ya mafunzo hayo na mikakati ya serikali ili kufikia adhima ya ongezeko la uzalishaji