Radio Fadhila

Watu wasiojulikana wachoma vifaa kanisani Masasi

30 April 2025, 5:34 PM

Eneo ambalo baadhi ya vifaa vilikusanywa na kuchomwa moto. Picha na Lilian Martin

Haya ni mambo yanayojili katika jamii zetu na katika yote hivyo nawasamehe wale wote waliotenda hayo yamkini si akili yao

Na Lilian Martin

Watu wasiojulikana wamevamia katika kanisa Anglikana lililopo kijiji cha Mpeta wilayani Masasi mkoani Mtwara na kukusanya baadhi ya vitu kama mavazi ya misa,membari, vitambaa vya mapambo ya madhabahuni, na memberi kisha kuviweka juu ya madhabahu na kuvichoma moto.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia April 30, 2025 majira ya saa 6 usiku ambapo watu hao waliingia kanisani hapo na kuchoma moto baadhi ya vitu, ambapo baadhi ya mashuhuda wameeleza kuwa vitu vingine vimeonekana porini vikiwa vimetupwa, hivyo si rahisi kugundua kama watu hao ni wakazi wa eneo hilo au wametoka mbali na eneo hilo. huku.

Akizungumzia tukio hilo kiongozi wa Kanisa hilo Padre Edward Valentino amesema amesikitishwa na tukio hilo la kuchoma vifaa vifaa huku akiiomba jamii kujitokeza katika urejeshaji wa vifaa hivyo ili kanisa liendelee na huduma zake.

Sauti ya Padri Edward Valentino

Sambamba na hayo, Padre Valentino aimeiasa jamii kuacha tabia hiyo ya kufanya matukio ya ajabu kwenye nyumba za ibada na maeneo mengine, huku akisema kuwa amewasamehe waliofanya tukio hilo kwa kile ambacho ameeleza kuwa huenda waliotekeleza tukio hilo si kwa akili zao.

Sauti ya Padri Edward Valentino