Radio Fadhila

Mabadiliko tabianchi chanzo shughuli za binadamu

14 February 2025, 11:45 AM

Katika ni afisa ugani kutoka TFS kanda ya kusini

Na lilian Martin

picha na Godbless Lucius

Katika kuadhimisha siku ya Radio Duniani kulikuwa na kaulimbiu inayosema Radio na badiliko ya tabia ya nchi hivyo wadau kutoka TFS ikiongozwa na Afsa ugani kanda ya kusini {Lindi,Mtwara,na Ruvuma} Bwan Anderson Besisila alizungumza kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi na chanzo chakena namna ya kukabiliana na hali hiyo ili kupunguza athari

katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika kituo cha Radio Fadhila Bwn Anderson alisema kuwa shughuli za binadamu ni chanzo kikubwa cha mabadiliko ya tabia ya nchi kutokana na shughuli zinazofanywa na binadamu ambazo zinasababisha kutoweka ka vitu vya asili

kutokana na kukua kwa miji na vijiji watu wanakata misitu kwa shughuli za kilimo wakati mwingine kwa ajili ya makazi, ujenzi wa viwanda pamoja na mifugo hivyo shughuli hizi zote husababisha upotevu wa miti hali inayopelekea hata upatikanaji wa maji kuwa mgumu kutokana na shughuli hizo zote amesema Besisila

pamoja na hayo pia aliwataka wananchi kujua kuwa wanalojukumu la kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwa ni pamoja na kupanda miti ili kukabiliana na changamoto hizo.