Wanafunzi Masasi wahimizwa kupambana na vitendo vya ukatili
17 November 2023, 9:55 AM
MASASI.
Mwenyekiti wa kampeni ya kupinga vitendo vya ukatili idara ye elimu mkoa wa Mtwara Kristine Simo, ambaye pia ni mwenyekiti wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Upendo Charity inayojishughulisha na kusaidia jamii yenye uhitaji iliyopo wilayani Masasi, amewataka wanafunzi wa shule ya msingi Mlimani iliyopo kata ya Migongo wilayani Masasi mkoani Mtwara kuwa mashujaa kwa kupaza sauti zao kwa kukataa kufanyiwa vitendo vya ukatili katika jamii wakiwemo watu wao wa karibu nyumbani.
Simo ametoa kauli hiyo alipotembelea Shuleni hapo pamoja na kuzungumza na Wanafunzi zaidi ya miatatu na baadhi ya Walimu wa Shule hiyo, kama sehemu ya kuunga mkono juhudi zinavyofanywa na Serikali katika kukemea na kupinga vitendo vya kikatili katika jamii.
Simo amesema ili kufikia malengo yao katika kusoma na kuja kuwa viongozi wakubwa katika nchi hii ni vizuri Watoto hao wakajenga hutamaduni wa kupinga vitendo hivyo kwa kujisimamia wenyewe pale wanapofanyiwa au kuona Mtoto mwenzao anafanyiwa kwa kutoa taarifa kwa walimu, polisi au kwao.
Pia Simo amesema wanafanya hivyo ili kuwasaidia kujakupata viongozi wazuri wenye sifa ambao watakuwa wanajitambua katika kutekeleza majukumu yao…………..insert.
Naye kwa upande wake Mjumbe wa kikundi cha Upendo charity Rukia Said maarufu kama Mama Mkamata Vyura amewahimiza wanafunzi kupenda kusoma zaidi na kuacha kujiingiza katika vitendo vya tamaa hasa wasichana jambo ambalo litapelekea ubakaji pamoja na kupachikwa mimba za utotoni katika umri mdogo chini ya miaka 18.
Aidha Rukia ametumia nafasi hiyo kuwakataza Wanafunzi kujiusisha kuingia katika mabanda ya video majira ya usiku kwani hayo nayo yamekuwa chanzo cha matukio ya kufanyiwa vitendo vya ukatili kwao…