Vyama vya ushirika Mtwara vyapigwa msasa kutumia mfumo mpya wa ‘MUVU’
12 June 2023, 12:23 PM
Takribani wajumbe 110 kutoka vyama vya ushirika wilaya za Masasi na Nanyumbu, wakiwemo makatibu, wahasibu na maafisi ushirika, wameshiriki katika mafunzo ya kujengewa uwezo wa kuendesha mfumo mpya wa ‘MUVU’ ili waweze kutekeleza majukumu yao kiufanisi na kidigitali zaidi.
Mfumo huo wa muvu ni mfumo ambao unatajwa kama mwarobaini wa kutatua changamoto mbalimbali za kimifumo ambazo hapo awali makatibu na wahasibu walikuwa wanakabiliana nazo na wakati mwingine kupelekea malalamiko wakati wa kuwahudumia wakulima, kutokana na kutokuwa na mfumo madhubuti katika kukidhi mahitaji ya wakulima.
Wakizungumza katika mahojiano na mwandishi wetu, baadhi ya washiriki walioshiriki katika mafunzo hayo, wameelezea matarajio yao kuhusu mafunzo hayo kwa kusema:
Mapema mrajisi wa vyama vya ushirika mkoa wa Mtwara Kakozi Ibrahim, akizungumza mbele ya wanahabari akaeleza malengo ya mafunzo hayo kwa kusema:
Kwa upande wake afisa tehama kutoka tume ya maendeleo ya ushirika Valentino Ngoda, ambaye alikuwa anaendesha mafuzo hayo akizungumza katika mahojiano pamoja na kueleza mengi akasema
Mafunzo hayo yaliyodumu kwa siku tatu yamepagwa kufanyika katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mtwara.