Jamii ya wafugaji Lukuledi wakosa chanjo ya UVIKO 19
29 March 2023, 10:13 AM
Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi inayosababisha jamii za wafugaji kuhamahama kutafuta malisho kumechangia kwa kiasi kikubwa kupelekea jamii kukosa kupata baadhi ya huduma za kijamii
Hayo yamesema na baadhi ya Jamii ya wafugaji ambao wanafanya shughuli zao za ufugaji wa kuhamahama katika maeneo ya Kata ya Lukuledi, Wilayani Masasi, Mkoani Mtwara, ambao wamekosa huduma ya chanjo ya Uviko 19
Wafugaji hao wa Jamii ya Wamaasai wamekiri kuwa kuishi kwao kwa muda katika makambi yao kumechangia kiasi kwamba hawajawaona watoa huduma ya UVIKO 19
Aidha, kutokana na kutokuwa na makazi maalumu kwa wafugaji hao, Diwani wa Kata ya Lukuledi, Hamza Said Kalembo, amesema kuwa wao hawana jamii ya wafugaji katika eneo lao japo amekiri kuwa alishawahi kuwaona wakipita wakati fulani wakiwa na mifugo yao
Kwa upande wake Mratibu wa Chanjo Msaidizi wa Halmashauri ya Mji Masasi, Benjamin Elius, amesema kuwa wao katika eneo lao wamefikia makundi mbalimbali na wafugaji wao hawajajitenga kwani wanawafikia na hawahitaji huduma za kipekee na ni wadogo wadogo na wanafugia ndani