Mapadre na Watawa waombwa kutumia hekima na busara
4 February 2023, 11:08 AM
Na Lawrence Kessy
Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Mhashamu Askofu Lazarus Vitalis Msimbe, SDS amewaomba mapadre na watawa kutumia hekima na busara za mababa wa Kanisa waliobobea kupitia maandiko mbalimbali ili wapate miongozo ili kupata uzoefu katika maisha ya kiroho.
Utawa ni wito wa makutano kati ya yesu na watawa pamoja na wote waliojitoa na kuwekwa wakfu kwa ajili ya kumtumikia Mungu na wanadamu.
Askofu Msimbe amyaesema hayo wakati katika homilia yake kwenye adhimisho la Misa Takatifu ya utoaji wa daraja takatifu la Upadre kwa Mashemasi wawili wa Shirika la Mungu mwokozi – Wasalvatoriani iliyofanyika katika Kanisa la Chuo Kikuu Kishiriki cha Jordani Jimboni Morogoro
Aidha Askofu Msimbe amewaomba Watawa kuruhusu Nuru ya yesu ipenye ndani mwao ili iweze kubadilisha maisha yao kwa ajili ya kujitakatifuza na kumtumikia Mungu kwa uaminifu na ukamilifu kupitia daraja hiyo ya Upadre ambayo ni zawadi kutoka kwa mama kanisa.
Askofu Msimbe amesema kuwa wito wa utawa ni wito wa makutano kati ya yesu na watawa pamoja na wote waliojitoa na kuwekwa wakfu kwa ajili ya kumtumikia Mungu na wanadamu
Aidha amesema kuwa yeyote anayetaka kuwa mfuasi wa Yesu kamwe hawezi kukwepa mateso kwa sababu Kristo aliyewaita katika wito huo aliteseka na kufa Msalabani kwa sababu ya Ukombozi wa dunia, hivyo wakithubutu kukwepa mateso wanaweza kupoteza waamini wengi.
Zingatieni nadhiri ya utii kwa kuwa yeyoye atakayeshindwa kuzingatia nadhiri hiyo ni rahisi sana kuanguka.
Hata hivyo amewaomba Mapadre wapya Pd. Michael Henerico, SDS na Lazarus Nyang’au Motii, SDS wajitahidi kuishi kwa uaminifu maisha ya wakfu katika Kanisa, hasa kwa kuzingatia nadhiri zao za utii, ufukara na usafi kamili wa moyo kwa ajili ya kumpendeza Mungu
Amewaomba Mapadre hao kuzingatia nadhiri walizoweka ili ziweze kuwafikisha kwenye utakatifu wa kweli na kupata nguvu ya kuwapeleka wengine kwenye wokovu wa maisha ya milele, huku wakijitahidi zaidi kuwa makini na nadhiri ya utii kwa kuwa yeyoye atakayeshindwa kuzingatia nadhiri hiyo ni rahisi sana kuanguka
Sambamba na hayo amewaomba watawa wajifunze kupitia uzoefu wa watengine kupitia maisha