Wanafunzi wapewa elimu ya usalama barabarani
31 January 2023, 12:04 PM
Inspekta Magazi akiwa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtapika wakati akiwapa elimu ya usalama barabarani kipengele cha waenda kwa miguu.
Na Lawrence Kessy
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtapika, iliyopo Kata ya Mwenge Mtapika, Halmashauri ya Mji wa Masasi, Wilayani Masasi, Mkoani Mtwara wametakiwa kuwa mabalozi wazuri wa Usalama Barabarani baada ya kupewa Elimu.
Rai hiyo imetolewa na Inspekta wa Jeshi la Polisi, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Usalama Barabrani, Yona Magazi, kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilayani Masasi, wakati akifundisha wanafunzia hao somo la usalama barabarani, kipengele cha Usalama kwa waenda kwa Miguu.
Inspekta Yona akizungumza katika sehemu ya kuwashukuru mara baada ya kukamilisha kwa somo hilo amewaomba wanafunzi hao wazingatie elimu hiyo na kanuni alizowapatia kwa ajili ya kuokoa maisha yao na wengine.
“Naomba nanyi mkawe mabalozi wa usalama barabarani kwa kuwaelimisha wengine hasa pale mnapoona wakiwa katika mazingira ambayo ni hatarishi barabarani”, amesema Inspekta Magazi.
“Naomba nanyi mkawe mabalozi wa usalama barabarani kwa kuwaelimisha wengine hasa pale mnapoona wakiwa katika mazingira ambayo ni hatarishi barabarani”, amesema Inspekta Magazi.