Shule jumuishi Ya Mfano Ya Msingi Lukuledi Imeziduliwa!!!
16 January 2023, 10:07 AM
MASASI.
Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda amezindua Shule ya Msingi jumuishi ya mfano Lukuledi Wilayani Masasi mkoani mtwara ikiwa ndio shule ya kwanza ya mfano kwasasa ambayo huwezi kuiona sehemu nyingine Tanzani kwa ukubwa na wingi wa miundombinu huku akitoa pongezi kwa Mashirika yaliyowezesha ujenzi huo kukamilika kwake ambayo ni UNESCO,UNICEF na BANK YA DUNIA.
Shule hiyo ambayo inapokea Wanafunzi wenye ulemavu wa viungo na wale ambao wanaulemavu wa kutosikia Viziwi imejengwa kwa gharama ya Shilingi bilioni I.5, huku ikiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 480 kwa mkupuo mmoja.
Profesa Mkenda wakati akizundua shule hiyo ametumia nafasi hiyo kusisitiza jamii kutowafungia watoto wenye mahitaji maalumu badala yake wawapeleke shuleni kwani Raisi Samia Suluhu Hasani alishatoa agizo Watoto wote wapelekwe Shuleni na hasiachwe mtoto kwa sababu ya tatizo la ulemavu au kupata ujauzito wote wapatiwe fursa ya kusoma na ndio maana Serikali inajenga Shule kama hizo.
Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Chama Mapinduzi CCM, Wilayani Masasi Mariamu Kasembe akatumia nafasi hiyo kuiyomba Serikali iweze kuwajengea uzio watoto hao kama sehemu ya kulinda usalama wa wao.
Shule hiyo kwa sasa inawanafunzi wapatao 145 huku Wasichana wakiwa 71 na Wavulana 74.
Shule hiyo inaofisi sita, madarasa kumi na mbili, bwalo lenye uwezo wa kuhudumia Wanafunzi mia tatu likiwa limeambatanishwa na Jiko na Stoo , Mabweni manne yenye uwezo wa kuchukuwa Wanafunzi 480 yakiwa na vyumba maaalumu, Nyumba za Walimu tisa, na Jiko kwa ajili ya kupikia.