Kuelekea maadhimisho Ya Miaka 61 yaUhuru wa Tanzania Bara
9 December 2022, 6:19 AM
Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bi Claudia Kita inayoadhimishwa terehe 09 Disemba kila mwaka ameongoza Bonanza la Mpira wa Miguu lililoambatana na Ugawaji wa vifaa vya usalama barabarani kwa Madereva pikipiki (bodaboda), Kofia ngumu (HELMET) na Jaketi maalum za kuvaa waendesha pikipiki.
akizungumza wakati wa ugawaji wa vifaa hivyo kwa Bodaboda wapatao 30 Mkuu wa Wilaya Claudia Kitta amesema baadhi ya matukio na mapungufu yanayojitokeza kwenye jamii yanasaidiwa na bodaboda kwani kuna baadhi yao wanakubali kuwasafilisha wahalifu kwa tamaa za pesa, amewataka wawe waaminifu na mabalozi wa kulinda amani.
Lakini pia amesema kwa sasa Kama Wilaya wapo kwenye kampeni ya kuhakikisha pikipiki ziwe kama zilivyotoka kiwandani kwani kuna baadhi ya bodaboda wamekua wakipunguza ubora na thamani ya pikipiki kwa kuzitoa Side mirror.