Mwenge Wa Uhuru Wa Zindua Miradi Mbalimbali Ndani Ya Wilaya Ya Masasi Leo.
31 August 2021, 2:14 PM
Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Luteni Mwambashi amegiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa Jengo la utawala Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoa wa Mtwara linalojengwa maeneo ya Mbuyuni .
Mwambashi ameyasema hayo wakati wa kukagua ujenzi huo katika Mbio za Mwenge na kuwataka TAKUKURU kumfanyia uchunguzi kabla ujenzi huo haujaendelea .
Mradi huo unagharibu sh. Billion 2.8 lakini Hadi hatua iliyofikia imegharimu sh Million mia Saba ,hivyo amemtaka Mkuu wa wilaya hiyo na Taasisi ya kupambana na Rushwa TAKUKURU kuwa Makini na kuchunguza mwendo wa Miradi na kuhakikisha inaendana na Gharama zilizowekwa katika utekelezaji.
Na katika hatua nyingine Luten Mwambashi amekataa kuweka Jiwe la Msingi ujenzi wa Wodi 3 katika Hospital ya Wilaya ya Masasi iliyopo Makao Makuu ya wilaya hiyo Mkoani Mtwara.
Luteni Mwambashi amesema kuwa katika kukagua nyaraka zote za Mradi zinanyesha haziko sahihi Kwa sababu ujenzi huo umegharimu sh Million 500 lakini baada ya uchunguzi uliofanyika ndani ya masala mawili kiasi Cha sh Million 11 zimepotea na Taarifa inaonyesha Hadi ujenzi ulipofikia imetumika sh Million 411.