Mazalia ya mbao maarufu kama rapurapu kutumika mkaa!!
17 July 2021, 5:03 AM
Huu ni mkaa ambao umetengenezwa kutokana na mazalia ya mbao maarufu kama rapurapu baada ya mbao kurandwa mkaa huu unasifa bora ya unapotumia kwanza unatumia kiasi kidogo sana cha lakini pia unasifa ya kuwaka kwa muda mrefu tofauti na mkaa tuliyouzowea.Mkaa huu unatengenezwa na kampuni ya Kushoko kutoka Tabora lakini ambayo imeamua kuja kufanya kazi wilayani Masasi mkoani Mtwara .
Kampuni hii kazi yake kubwa ni kwa sasa ni kutengeneza Mashine ambazo zinachakata mazalia mbalimbali ya mazao ya chakula na misitu kuwa mkaa bora badala ya mazalia hayo kutupwa kama tulivyozoea.Baada ya Mashine hizo kutengenezwa zinauzwa kwa yoyote anayotaka kununua kwani zitakuwezesha kuanza kuwa mjasiliamali bora ambaye utakuwa na fursa pia ya kujitengenezea kipato kikubwa.
Wataalamu hawa licha ya kukuuzia Mashine hizi pia watakupa utaalamu wa namna ya kutengeneza mkaa mbadala kwa kutumia Mashine hizo.Kampuni unafanya kazi zake maeneo ya Maliasili mpya wilayani Masasi
Kazi hii mazuri inayofanywa na kiwanda hiki kidogo ilifanya mkuu wa wilaya ya Masasi , Claudia Kitta kwenda kujionea mwenyewe kazi hayo na kuwapongeza wahusika na kutoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Masasi kujitokeza kwenda kujipatia Mashine hizo ili kujishughulisha na shughuli za ujasiliamali.