Yusuphu Namnila Ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kutenga bajeti ya pembejeo kwa ajili ya Wakulima wa zao la korosho
21 April 2021, 1:08 PM
Mwenyekiti wa chama Cha Ccm Mkoa wa mtwara Yusuphu Namnila ,Ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kutenga bajeti ya pembejeo kwa ajili ya Wakulima wa zao la korosho,Nakuwaomba Wakulima kupokea kwa kile kilichoratibiwa na kukifanyia kazi ,Na kujiuliza kwanini uzalishaji wa zao Hilo umeshuka kwackiasi kikubwa Mkoa wa Mtwara tofauti na kipindi Cha nyuma na kuwaomba bodi ya korosho ,Serikali na Wakulima wenyewe kuliangalia kwa pamoja .
Ameyasema hayo Leo hii katika Mkutano wa 21 wa bodi ya Mamcu uliofanyika Mkoani Mtwara ukumbi wa chuo Cha Ualimu ambao ulishiriki Wajumbe wa chama Cha ushirika Mamcu na viongozi mbalimbali kwa lengo la kuchagua viongozi watakaosimamia bodi ya chama kikuuu na kuwaomba wajumbe walioshiriki uchaguzi kuchagua viongozi sahihi ambao wataleta mafanikio katika chama .
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mtwara Dustan Kyoba ametoa pongezi kwa bodi inayomaliza mda wake kwa kazi ambayo wameifanya kwa kipindi Chao na kuwataka viongozi wapya watakaochaguliwa kuwa waaminifu ili kuongeza uzalishaji wa zao Hilo.
Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa wa mtwara Gelasus Biakanwa amewapongeza chama Cha Ushirika Mamcu kwa kuanzisha miradi Yao na kuwataka viongozi wapya watakaochaguliwa kuendekeza miradi hiyo na kuongeza miradi mwingine .
Pia kupitia Mkutano huo Biakanwa alieleza changamoto ambazo zinasababisha kushuka kwa zao la korosho Mkoa wa mtwara.
story – rabia nandonde